JEE! BIBLIA YA RUHUSU KUNUNUA NA KUUZA WATUMWA

JEE!  BIBLIA YA RUHUSU KUNUNUA NA KUUZA WATUMWA !

Soma Kutoka 21 : 7 – 9 ” Mtu akimwuza binti yake awe kijakazi, hatatoka yeye kama watumwa wa kiume watokavyo.

Kwamba bwana wake hakupendezewa naye, akiwa amemposa, ndipo atakubali akombolewe; hana amri yeye kumwuza aende kwa watu wageni maana amemtenda kwa udanganyifu.

Kwamba amposa mwanawe, atamtendea kama desturi zipasazo binti zake.”

Yakobo alikuwa na watumwa ! Soma Mwanzo 32: 13 – 18 ” Akakaa huko usiku ule. Kisha akatwaa baadhi ya vitu alivyokuwa navyo, kuwa zawadi kwa Esau, nduguye;

mbuzi wake mia mbili, na mbuzi waume ishirini, kondoo wake mia mbili, na kondoo waume ishirini;

ngamia wanyonyeshao thelathini pamoja na wana wao, ng’ombe wake arobaini na mafahali kumi; punda wake ishirini na wana wao kumi.

Akawatia mkononi mwa watumwa wake, kila kundi peke yake. Naye akawaambia watumwa wake, Vukeni mbele yangu, mkaache nafasi kati ya kundi na kundi.

Akamwagiza yule wa kwanza akasema, Esau, ndugu yangu, akikukuta, na kukuuliza, akisema, Wewe u wa nani? Unakwenda wapi? Tena ni wa nani hawa walio mbele yako?

Basi, useme, Ni wa mtumwa wako, Yakobo, ni zawadi, aliyompelekea bwana wangu, Esau. Na tazama, yeye mwenyewe yuko nyuma yetu

Daudi alikuwa anamiliki watumwa mia sita ! (600) ! Soma 2 Samueli 15 : 14 – 18 “Salomono alikuwa na watumwa mamia ! Angalia ! 1 Wafalme 9 : 20 – 22

ADHABU YA KUMPIGA MTUMWA INARUHUSIWA NA YEHOVA ! Soma Kutoka 21 : 20 – 21 ” Mtu akimpiga mtumwa wake, au kijakazi chake, kwa fimbo, naye akifa mkononi mwake, hana budi ataadhibiwa.

Lakini akipona siku moja au mbili hataadhibiwa; maana, ni mali

Luka 12 : 47 – 48 “

KUPORA KATIKA BIBLE

“Nao wakatwaa hizo nyara zote, na mateka yote, ya wanadamu na ya wanyama.

Nao wakawaleta mateka ya wanadamu, na mateka ya wanyama, na hizo nyara, na kuyaweka mbele ya Musa, na mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya mkutano wa wana wa Israeli, hapo maragoni katika nchi tambarare za Moabu, zilizo karibu na Yordani hapo Yeriko.”

Hesabu 31: 11 – 12

Mungu anamfanya Musa kamaMUNGU ?

“Bwana akamwambia Musa, Angalia, nimekufanya wewe kuwa kama Mungu kwa Farao; na huyo ndugu yako Haruni atakuwa nabii wako.”

Kutoka 7 : 1

MWANAMKE NA HEDHI

“Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia,

Nena na hao wana wa Israeli, uwaambie, Mwanamke akitunga mimba na kuzaa mtoto mume, ndipo atakuwa yu najisi siku saba; kama katika siku za kutengwa kwake kwa ajili ya hedhi, ndivyo atakavyokuwa najisi.

3Siku nane mtoto atatahiriwa govi ya zunga lake.

Na huyo mwanamke atakaa katika damu ya kutakata kwake siku thelathini na tatu; asiguse kitu kilicho kitakatifu, wala asiingie mahali patakatifu, hata siku hizo za kutakata kwake zitakapotimia.”

Walawi 12 : 1 – 4

IKIWA BIBLIA NI NENO LA MUNGU KWA NINI NDANI YAKE MNA KHITILAFU NYINGI ?

1. Kabla ao baada ?

Tufunue Mwanzo 1 : 20 – 25 Hapa mwandishi anatueleza kwamba Yehova aliumba wanyama kabla ya kuumbwa mtu.

Tulinganishe na Mwanzo 2 : 18 – 20

Katika andiko hii, mwandishi huyu anajipinga tena kwa kutupa habari kwamba wanyama waliumbwa baada ya Yehova kuumba mtu !

2. 2 ao 7 ?

Tuangalie Mwanzo 6 : 19 – 21

“Hapa tunaoneshwa kwamba Nuhu aliagizwa na Mwenyezi Mungu kwamba kila kitu kilicho hai ya miili yote, italetwa wawili wawili wa kila namna katika safina. Ebu

Tulimganishe na Mwanzo 7 : 2 – 3

” huku mwandishi anasema kinyume na maandiko hapo juu ! – Anatufunza kwamba Mwenyezi Mungu aliagiza Nuhu achukue katika safina kila kitu kilicho hai ya miili yote saba saba !

Sehemu ipi tufate ?

3. 70 ao 75 ?

Na nafsi zile zote zilizotoka viunoni mwa Yakobo zilikuwa ni nafsi sabini; na huyo Yusufu alikuwa huko ndani ya Misri tangu hapo.”

KUtoka 7 : 1 – 5

Tulinganishe na Matendo ya mitume 7 : 14

“Yusufu akatuma watu akamwita Yakobo babaye na jamaa zake wote pia, watu sabini na watano.”

– Agano la Kale yazungumzia kwamba jamaa ya Yakobo ni watu 70

– Agano jipya imetueleza kwamba ni watu 75.

Tunajiswali :

a) Ipi tufuate baina ya hivi viwili ?

b) Je Roho Takatifu ilijipinga ?

c) Sehemu gani hasa iliandikwa ikiongozwa na Roho Takatifu ?

4. 3300 ao 3600 ?

1 Wafalme 5 : 16

” mbali na maakida yake Sulemani waliokuwa juu ya kazi, elfu tatu na mia tatu, wasimamizi wa watu waliotenda kazi.’

Linganisha na 2 Mambo ya Nyakati 2 : 2

” Sulemani akahesabu watu sabini elfu wawe wachukuzi wa mizigo, na watu themanini elfu wawe wachongaji milimani, na elfu tatu na mia sita wawe wasimamizi wao.”

Wachungaji mutujibu jamaani ! 

5. 3 ao 7 ?

Angalia 1 Mambo ya Nyakati 21 : 11 – 12

” Basi Gadi akamwendea Daudi, akamwambia, Bwana asema hivi, Kubali upendavyo;

miaka mitatu ya njaa; au miezi mitatu kuangamia mbele ya adui zako, ukipatwa na upanga wa watesi wako; au siku tatu upanga wa Bwana, yaani tauni katika nchi, na malaika wa Bwana akiharibu kati ya mipaka yote ya Israeli. Haya basi ufikiri ni jawabu gani nimrudishie yeye aliyenituma.”

Linganisha na 2 Samueli 24 : 13

” Basi Gadi akamwendea Daudi, akamweleza, akamwambia, Basi, miaka saba ya njaa ikujie katika nchi yako? Au miezi mitatu ukimbie mbele ya adui zako, huku wakikufuatia? Au siku tatu iwe tauni katika nchi yako? Fanya shauri sasa, ufikiri, ni jawabu gani nimrudishie yeye aliyenituma.”

Swali :

Sehemu gani tufuate ?

6. 1700 ao 7000 ?

Twendee 2 Samueli 8 : 4 

” Daudi akampokonya wapanda farasi elfu na mia saba na askari waliokwenda kwa miguu ishirini elfu; Daudi akawakata mshipa farasi wote wa magari, ila farasi wa magari mia akawasaza.”

Linganisha na 1 Mambo ya Nyakati 18 : 4

” Daudi akampokonya magari elfu, na wapanda farasi saba elfu, na askari waendao kwa miguu ishirini elfu; Daudi akawakata mshipa farasi wote wa magari, ila wa magari mia akawaweka.’

Swali yanatokea :

Je, Roho Takatifu aliwaongoza waandishi hawa ao la ? 

7. 700 ao 7000 ? 

Katika 2 Samueli 10 : 17 – 18

– Tunaambiwa kwamba Daudi aliwaua watu wa magari mia saba (700) na waaskari wa migu elfu arubaini (40.000). Linganisha na 1 Mambo ya Nyakati 19 : 18 hapa mwandishi huyu anazungumzia kwamba Daudi aliwaua watu wa magari elfu saba (7000) na watu wenye kwenda kwa miguu elfu arubaini (40.000).

8. – 100.000 ao 800.000 ? 

– 470.000 ao 500.000 ?

2 Samueli 24 : 9

– Tumeona kitabu cha Samueli inatufundisha kwamba Yoabu alitolea mfalme jumla ya watu waliokuwa katika Israeli ni elfu mia nane (800.000) wenye panga na watu wa Yuda walikuwa watu elfu mia tano (500.000).

Tazama 1 Mambo ya Nyakati 21 : 5 hapa hesabu ni kinyume na yaliyotolewa na kitabu cha Samueli. Hesabu aliyotoa Yoabu ni elfu mia moja (100.000) wenye kuvuta upanga na Yuda walikuwa elfu mia nne na sabini (470.000) wenye kuvuta upanga.

9. 22 ao 42 ?

Tuangalie 2 Wafalme 8 : 26

” Ahazia alikuwa na umri wa miaka ishirini na miwili alipoanza kutawala; akatawala mwaka mmoja huko Yerusalemu. Na jina la mamaye aliitwa Athalia binti Omri mfalme wa Israeli.”

Linganisha na 2 Mambo ya Nyakati 22 : 2

” Ahazia alikuwa na umri wa miaka arobaini na miwili alipoanza kutawala; akatawala mwaka mmoja huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Athalia binti Omri.”

Tunalo swali :

Sehemu gani ifuatwe ?

10. Nani alimuagiza Daudi kwa kuhesabu Waisraeli ?

Tufunue 2 Samueli 24 : 1

“Tena hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, akamtia Daudi nia juu yao, akisema, Nenda, ukawahesabu Israeli na Yuda.”

Linganisha na 1 Mambo ya Nyakati 21 : 1

“Tena shetani akasimama juu ya Israeli, akamshawishi Daudi kuwahesabu Israeli.”

Swali tunalo :

Sehemu ipi ya kufuata ?

11. Waamuzi 1 : 1 ” Ikawa baada ya kufa kwake Yoshua, wana wa Israeli wakamwuliza Bwana, wakisema, Ni nani atakayekwea kwanza kwa ajili yetu juu ya Wakanaani, ili kupigana nao ?”

Tulinganishe na Waamuzi 2 : 8 ” Kisha Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Bwana, akafa, naye alipata umri wa miaka mia na kumi. 

12. WANA WA ZATU NI WA NGAPI ?

Ezra 2 : 8

” Wana wa Zatu, mia tisa arobaini na watano.”

Linganisha na Nehemia 7 : 13

” Wana wa Zatu, mia nane arobaini na watano.” 

Swali linakuja :

Sehemu ipi tufuate ?

13. WANA WA ADINI NI WANGAPI ?

Ezra 2 : 15

“Wana wa Adini, mia nne hamsini na wanne.

Linganisha na Nehemia 7 : 20

” Wana wa Adini, mia sita hamsini na watano.

14. 200 ao 245 ?

Ezra 2 : 65

– Katika andiko hili, tunaona kwamba jumla ya waimbaji waliotajwa hapa ni mia mbili (200).

Tutupe jicho katika Nehemia 7 : 67

Hapa anasema kwamba waimbaji ni yapata mia mbili arubaini na tani (245) !

15. WANA WA HASHUMU NI WANGAPI ?

Nehemia 7 : 22

” Wana wa Hashumu, mia tatu ishirini na wanane. 

Linganisha na Ezra 2 : 19

” Wana wa Hashumu, mia mbili ishirini na watatu.”

Swali linakuja :

Tukazane tu kusema kwamba waandishi hawa waliongozwa na Roho Takatifu ?

16. 2499 ao 5400 ?

Mwandishi huyu ametowa hesabu ya vyombo vya fedha na zahabu kama hivi :

– sahani ya zahabu 30

– sahani ya feza 1000

– visu 29

– mabakuli ya zahabu 30

– mabakuli ya feza 410

vyombo vingine 1000

kwa jumla (total) 2499

Mwandishi huyu ametowa jumla ya yote ni 5400 ! Kinyume na hesabu tuliopata hapo juu (2499).

17. JE ! YUSUFU NI MWANA WA YAKOBO AO MWANA WA ELI ?

Tuchunguze Matayo 1 : 16

“Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo.”

Tulinganishe na Luka 3 : 23

” Na Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa amepata umri wake kama miaka thelathini, akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu, wa Eli,”

Swali yanatokea :

Sehemu gani iliongozwa na Roho Takatifu ?

18. Walipeleka habari mjini ao la ?

“Wakaondoka kaburini, wakarudi; wakawaarifu wale kumi na mmoja na wengine wote habari za mambo hayo yote.”

Luka 24 : 9

Linganisha na Marko 16 : 8

“Wakatoka nje, wakakimbia kutoka kaburini; kwa maana wameingia tetemeko na ushangao; wala hawakumwambia mtu neno, maana waliogopa.”

Mwandishi wa kitabu cha Marko anatufundisha kwamba baada ya kutoka kaburini hawakumwambia mtu neno.

Lakini mwandishi wa kitabu cha Luka anaeleza kinyume na kutufahamisha kwamba waliarifu habari hiyo !

Maswali yanakuja :

a) Sehemu gani hasa iliandikwa ikiongozwa na Roho Takatifu ?

b) Tukazane tu kuita maandishi haya kuwa ni takatifu ?

19. Wakati gani alikwenda ao walikwenda kaburini ?

Marko 16 : 1 – 2

” Hata sabato ilipokwisha kupita, Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Yakobo, na Salome walinunua manukato wapate kwenda kumpaka.

Hata alfajiri mapema, siku ya kwanza ya juma, wakaenda kaburini, jua lilipoanza kuchomoza;”

Linganisha na Yohana 20 : 1

“Hata siku ya kwanza ya juma Mariamu Magdalene alikwenda kaburini alfajiri, kungali giza bado; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini” 

Mwandishi wa kitabu cha Marko anasema kwamba Maria Magdalena na wenzake walienda kaburini asubui mapema sana siku ya kwanza ya juma wakati JUA LILIPOCHOMOZA.

Lakini mwandishi wa kitabu cha Yohana anapinga kabisa habari hiyo; anatueleza kwamba Maria Magdalena alienda kaburini pekee yake asubui mapema INGALI GIZA BADO !

Swali tunalo :

a) Ipi tufuate baina hivi viwili ?

b) Je Roho Takatifu ilijipinga ?

20. YUDA ALIKUFA VIPI ?

Matayo 27 : 5

” Akavitupa vile vipande vya fedha katika hekalu, akaondoka; akaenda, akajinyonga.

Linganisha na

Matendo ya mitume 1 : 18

“Basi mtu huyu alinunua konde kwa ijara ya udhalimu; akaanguka kwa kasi akapasuka matumbo yake yote yakatoka.”

Swali yanatokea :

Ni Roho Takatifu gani alimuongoza mwandishi wa kitabu cha Matayo aandike kwamba Yuda alijinyonga; na ni Roho Takatifu gani alimongoza mwandishi wa kitabu cha Matendo ya mitume aandike kwamba Yuda alianguka chini na akapasuka matumbo ?

21. Nani alibeba msalaba kwenda Golgotha ?

Matayo 27 : 32 – 33

” 32 Hata walipokuwa wakitoka, wakamwona mtu Mkirene, jina lake Simoni; huyu wakamshurutisha auchukue msalaba wake.

Na walipofika mahali paitwapo Golgotha, yaani, Fuvu la kichwa,”

Linganisha na Yohana 19 : 16 – 17

” 16 Basi ndipo alipomtia mikononi mwao ili asulibiwe; nao wakampokea Yesu.

17 Akatoka, hali akijichukulia msalaba wake, mpaka mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, au kwa Kiebrania, Golgotha.”

Tunajiswali : 

Ni Roho Takatifu gani alimwongoza mwandishi wa kitabu cha Matayo aseme kwamba aliyebeba msalaba mpaka Golgotha ni Simoni Mkurene. Na ni Roho Takatifu gani alimwongoza mwandishi wa kitabu cha Yohana atuelezee kwamba aliyebeba msalaba mpaka Golgotha ni Masihi mwenyewe.

22. 1 ao 2 ?

Tazama Luka 23 : 39 – 40

“Na mmoja wa wale wahalifu waliotungikwa alimtukana, akisema, Je! Wewe si Kristo? Jiokoe nafsi yako na sisi.

Lakini yule wa pili akamjibu akamkemea, akisema, Wewe humwogopi hata Mungu, nawe u katika hukumu iyo hiyo ?”

Linganisha na Matayo 27 : 44

” Pia wale wanyang’anyi waliosulibiwa pamoja naye walimshutumu vile vile.”

Mwandishi wa kitabu cha Luka anasema kwamba ni mnyanganyi mmoja ndiye alimtukana Masihi. Kinyume na mwandishi wa kitabu cha Matayo ambaye anatueleza kwamba ni wawili ndio walimtukana Yesu.

23. SAA TATU AO SAA SITA ?

Funua Marko 15 : 25 – 27 ” 25 Basi ilikuwa saa tatu, nao wakamsulibisha.

26 Palikuwa na anwani ya mashitaka yake iliyoandikwa juu, MFALME WA WAYAHUDI.

27 Na pamoja naye walisulibisha wanyang’anyi wawili, mmoja mkono wake wa kuume na mmoja mkono wake wa kushoto.”

Linganisha na Yohana 19 : 14 “Nayo ilikuwa Maandalio ya pasaka, yapata saa sita. Akawaambia Wayahudi, Tazama, Mfalme wenu !

Swali tunalo : Ni Roho Takatifu gani ndiye alimwongoza mwandishi wa kitabu cha Marko aandike kwamba SAA TATU walimsulubisha Yesu; na ni Roho Takatifu gani alimwongoza mwandishi wa kitabu cha Yohana atueleze kwamba SAA SITA Yesu anahukumiwa mbele ya Pilato na hajafikishwa bado msalabani ao juu ya mti ?

24. KABLA AO BAADA ?

Angalia Luka 23 : 45 “jua limepungua nuru yake; pazia la hekalu likapasuka katikati.

46 Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu.”

Linganisha na Marko 15 : 37 – 38 ” Naye Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho.

Pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini.”

Swali linakuja : Ni Roho Takatifu gani ilimwongoza mwandishi wa kitabu cha Marko atufahamishe kwamba pazia la hekalu lilipasuka baada ya Yesu kukata roho ! Na ni Roho Takatifu aliongoza mwandishi wa kitabu cha Luka atueleze kwamba pazia la hekalu lilipasuka kabla ya Yesu kutoa roho ?

25. Kuchukuwa gongo na viatu ao kutochukuwa ?

Matayo 10 : 9 – 10

Mwandishi huyu anatueleza kwamba Masihi aliamuru wafuasi wake wasichukue kitu njiani, wala zahabu, wala feza, wala shaba ndani ya mishipi, wala mfuko kwa safari, wala kanzu mbili, wala viatu, wala gongo.

Lakini Marko 6 : 7 – 8 analeta habari nyingine kinywani mwa Masihi kwamba aliwaagiza wafuasi wake wasichukue kitu njiani ila gongo na kuvaa viatu.

26. 6 ao 8

Matayo 16 : 28…; 17 : 1 – 2

Siku sita baadaye

Linganisha na Luka 9 : 27 – 29

Siku nane baadaye

Swali linakuja : sehemu ipi ifuate ?

N.B. Kuna mengine mengi zaidi ya haya !!!

This topic was created and posted online by Mohsin  Farati Mohsen

Leave a comment