VITA VYA MSALABA

HISTORIA KUNAKO UISLAAM HUKO ULAYA JINSI ULIVYOKABILIANA NA VITA VYA MSALABA.

                       Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu.                        

                                   Assalaam Alaikum Warahmatullah Taala Wabarakaatuh

                                    

Barani Ulaya katika kipindi cha karne ya tano hadi kumi na tano, kinajulikana kama kipindi cha karne za kati,Miongoni mwa mambo yaliyo tawala katika kipindi hicho ni:Utawala wa kanisa juu ya jamii ya Ulaya na uzingatiaji wake mdogo juu ya masuala ya elimu na maisha ya kawaida ya watu, kwa kuenea Ukristo katika nchi za Ulaya,viongozi wa Ki-kristo pia walipata nafasi maalum katika nchi hizo nahivyo kudhibiti pande za maisha ya wakazi wa nchi hizo,

UwezowaviongoziwakanisanahasaMapapawakanisa Catholic uliongezekakwakiwangokikubwatokeakarneyatano (5) kiasikuahataWafalme waliokua wakitawazwa katika zama hizo walivishwa mataji yao ya ufalme na Mapapa

 

kwa msingi huo utawala mkali sato ya viongozi hao wa kanisa ulioandamana na uenezwaji wa fikra na mila potofu uliongezeka mara dufu barani Ulaya,na hivyo kuandaa uwanja wa kubaki nyuma kijamii,kisiasa,kiuchumi,kielimu na kiutamaduni katika jamii za Ulaya.

Miongoni mwa sifa zingine za karne ya kati ilikua ni utawala wa jamii za kikabila ambazo zilimiliki ardhi madaraka na utajiri mkubwa katika kipindi hicho, kila jamii ya kikabila ilikua na idadi ya wakulima na askari ambapo ilijijengea ngome na kua na utawala huru uliojitawala na kujiendeshea mambo yake yenyewe.

Kwa kawaida jamii hizo zilikua zikishiriki kwenye vita na kutumia wakati wao mwingi kuwaudhi na kuwashambulia watu wengine, mwanzoni mwa karne ya 8 au mwishoni mwa miaka ya karne ya kwanza ya Ki-islamu, Waislamu waliingia barani Ulaya ikiwemo;                                                                                                                                                                                                                                                                           Hispania,Ufaransa n.k,Wakitokea Kaskazini mwa bara la Africa na kuasisi Serikali za Ki-islamu,   kwa msingi huo uwanja ulikua umeandaliwa kwa ajili ya watu wa Ulaya kufahamu na kunufaika na utamaduni wa Ki-islamu. Katika upande wa pili,mfalme wa Roma ya mashariki ambae alikua akikabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi, alichukua hatua ya kuvamia na kushambulia nchi za Ki-islamu kwa lengo la kupora utajiri wa Waisalamu

Ama hujuma iliofanywa na Wakristo dhidi ya Ulimwengu wa Ki-islamu ilianza mwaka 1097, kwa amri ya papa Arban wa pili, hujuma ambayo iliendelea hadi mwaka wa 1270,kwa lengo la kuteka Ardhi za Waislamu,Papa huyo alitoa amri ya kutekwa Baytul-Muqaddas ambayo ipo katika Ardhi za Palestina ya hii leo, kwa kisingizio kwamba sehemu hiyo takatifu palikua ni mahala alipozaliwa Nabii lssa masihi (A.S) yaani Yesu Kristo, vita hivyo vilijulikana kwa jina la Msalaba kutokana na kua askari wa Ki-kristo walishambulia mji mtakatifu wa Baytul-Maqdis huku wakichora alama ya misalaba kwenye vifua vyao.

Katika vita hivyo askari hao wa hujuma walishambulia na kuharibu kabisa majengo ya Waislamu pamoja na kuwaua wengi miongoni mwao,kwa mfano; mwaka 492 Hijria,sawa na mwaka 1099 Miladia,wakati ambao askari wa msalaba walipoingia katika Baytul-maqdis,askari hao walitekeleza kila jinai katika eneo hilo kwa kuua kinyama kila Muislamu alieonekana mbele yao.

Waliwaua kinyama na kwa umati Waislamu wote waliokua wamekimbia na kujificha katika msikiti wa Qubbatus Sughraa, maulama na waja wengine watukufu wa M/Mungu waliuawa kikatili katika msikiti huo.

Askari hao wasio na chembe ya utu na huruma waliwakamata na kuwatupa ndani ya moto Waislamu wakiwa hai,

Will Darrant mwana Historia anaashiria mauaji hayo hayo ya kinyama yaliyofanywa na askari hao wa Msalaba katika jalada lake la (4) katika kitabu chake kiitwacho KISA CHA UTAMADUNI, au ( THE STORY OF CIVILISATION ) anamnukuu kasisi Ramon akisema

Kuhusiana na vita vya kwanza vya msalaba kua;(kulikua na Mandhari ya kutisha katika kila pande, kulikua na vichwa vilivyokatwa kutoka kwenyemiili ya Waislamu, baadhi ya makundi yalikatwa vichwa kwa kutumia mashoka na mingine kurushwa kutoka kwenye minara ya juu mirefu,na baadhi ya watu wengine waliteswa kwa siku kadhaa na kasha kuchomwa moto,kulikua na miguu na mikono ya viwiliwili vya Waislamu waliouawa iliotapakaa pote mitaani,kila sehem uliyoelekeza farasi wako ulikutana na viwiliwili vya watu waliouawa na mizoga ya farasi,

Kata kama vita vya msalaba hatimae vilimalizika kwa kushindwa watu wa Ulaya lakini hatimae Waislamu walijiandaa upya kwa ukamanda wa Swalehuddin Ayyubii na kuikomboa Baytul-maqdis baada ya kua mikononi mwa wavamizi wa vita vya msalaba,kwa muda wa miaka 90,na baada ya kuzikomboa nchi za Siria na Lebanoni na Misri,kufuatia kushindwa hukokukubwa kwa mara nyengine tena jeshi la msalaba lilijiandaa upya kukusanya askari wengi kwa lengo la kutaka tena kuivamia Baytul-maqdis,

Pamoja na kuendesha vita vikali dhidi ya Waislamu lakini hata hivyo wavamizi hao hawakufanikiwa kuutekatena mji huo mtakatifu,

Hatimae wavamizi hao walishindwa kabisa na kusalimu amri katika medani ya vita mwaka 1270,

Pamoja na kushindwa katika vita hivyo lakini bilashaka Wazungu walifaidika saana na kupata uzoefu mkubwa katika vita hivyo,walishuhudia na kunufaika na ustaarabu pamoja na maendeleo makubwa ya kiutamaduni ya Waislamu na hivyo kutambua kubaki kwao nyuma kielimu na kifikra wakilinganishwa na Waislamu, walipora na kutarjum vitabu vingi vya Waislamu katika taaluma mbali mbali zikiwemo za Falsafa Tiba Nyota na Nujumu Hisabati na Elimu nyenginezo nyingi

Wazungu pia waliweza kupata na kunufaika na elimu ya Waislamu katika Nyanja za utengezezaji karatasi na uzalishaji madawa na nyota na elimu nyingi kupitia miamala yao ya kibiashara na Waislamu,

Baadhi ya matokeo ya vita vya msalaba ni kutoweka kwa sato ya Mapapa na jamii za Ukabaila barani Ulaya,   kwamsingi huo wazungu waliweza kujiendeleza katika sekta mbalimbali za kielimu na utafutajio wa utajiri kwa uhuru kamili na bila kuhofia ukandamizaji wa kanisa,kwa utaratibu huo wazungu waliingia katika hatua mpya ya maendeleo ijulikanayo kama Belaysas.

 

Mwandishi wa makala hii ni:Suud Jaafar

Leave a comment