Unabii wa Paulo una utata

Utume wa Paulo

MT. 16:20 (SUV)

Ndipo alipowakataza sana wanafunzi wake wasimwambie mtu ye yote ya kwamba y eye ndiye Kristo. Ni kwa

Nini Yesu alikataa kuitwa Kristo?

Yesu alikataa kuitwa Kristo ni kwa sababu 2 ya 1 ni kuna mtu atajitokeza na kujiita yeye ni Kristo ( Yesu) yaani Yesu wa uongo, Wakrsito wana mtambua kuwa ni Anti Christ, Waislamu nao umtambua kwa jina la Masihidadjal (yaani Kristo wa uongo) lakini huwenda sababu kuu ni kwa ajili  Yesu alijua ya kwamba kutatokea mtu atakuja na kutumia neno la Kristo katika mahubiri yake. Tusome:

Mathayo: 24:4-6. Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganye.

5 Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi.

Basi tutazame ni nani aliye kuja na kumuita Yesu kwa kutumia hili neno KRISTO.

Matendo ya Mitume: 17:3-4 .akiyafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kwamba, Yesu huyu ninayewapasha ninyi habari zake ndiye Kristo

Matendo ya Mitume:18:5-6. Hata Sila na Timotheo walipotelemka kutoka Makedonia, Paulo akasongwa sana na lile neno, akiwashuhudia Wayahudi ya kwamba Yesu ni Kristo.

SASA WATU WA KAELEWA YALE YESU ALIYO YA SEMA katika aya ya 6 inasema:

6Walipopingamana naye na kumtukana Mungu, akakung’uta mavazi yake, akawaambia, Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu; mimi ni safi; tangu sasa nitakwenda kwa watu wa Mataifa.

Lakini hakuchoka, tusome:

Matendo ya Mitume:18:28.Kwa maana aliwashinda Wayahudi kabisa kabisa mbele ya watu wote, akionyesha kwa maneno ya maandiko ya kuwa Yesu ni Kristo.

Tumesha muona ambaye alikuja na kuhubiri watu ya kwamba Yesu ni Kristo.

Wasomaji wangu watadhani mimi ni mpigaji sana wa huyu Paulo, siyo bali nimesoma na kufuatiliya kwa undani utume wake Paulo ndiyo maana nimechukuwa fursa hii kuafikishiya nyinyi pia

Tutazame kwa undani UTUME wa Paulo ni kweli ni Mtume?

Matendo ya Mitume: 9:3-10………utakapofika kwenye aya ya 7 hapo Hight Light kwa kalam nyekundu ili usisahau inasema hivi:

Hata alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni. 4Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi? 5Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe. 6Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda. 7Na wale watu waliosafiri pamoja naye wakasimama kimya, wakiisikia sauti, wasione mtu. 8Sauli akainuka katika nchi, na macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski. 9Akawa siku tatu haoni; hali, wala hanywi.
10 Basi palikuwapo Dameski mwanafunzi jina lake Anania. Bwana akamwambia katika maono, Anania. Akasema, Mimi hapa, Bwana.

NOTE: 7 Na wale watu waliosafiri pamoja naye wakasimama kimya, wakiisikia sauti, wasione mtu.

(Walisekia Sauti, Lakini Hawakuona chochote yaani hawakuona Mtu ao Nuru )

Alikwenda kuwapasha habari hii watu

Matendo ya Mitume: 22:6-12 Utakapofika aya ya 9 hapo kuna utata inasema hivi:

6Ikawa nilipokuwa nikisafiri, nikikaribia Dameski, wakati wa adhuhuri, ghafula nuru kuu ilitoka mbinguni, ikanimulikia pande zote. 7Nikaanguka nchi, nikasikia sauti ikiniambia, Sauli, Sauli, mbona unaniudhi? 8Nikajibu, Wewe u nani, Bwana? Akaniambia, Mimi ni Yesu Mnazareti, ambaye wewe unaniudhi. 9Na wale waliokuwa pamoja nami waliiona ile nuru, lakini hawakuisikia ile sauti ya yule aliyesema nami. 10Nikasema, Nifanye nini, Bwana? Bwana akaniambia, Simama, uingie Dameski, na huko utaambiwa habari za mambo yote yaliyoamriwa uyafanye. 11Na nilipokuwa sioni kwa sababu ya fahari ya nuru ile, nikaongozwa na mikono yao waliokuwa pamoja nami, nikaingia Dameski.

NOTE: 9 Na wale waliokuwa pamoja nami waliiona ile nuru, lakini hawakuisikia ile sauti ya yule aliyesema nami.

Kauli mbili Tafuati, ya 1”Walisikia sauti , Hawakuona Mtu”.na tunapoliganisha na hapo awali Mdo:9:7 inasema: “Waliiona ile nuru, lakini Hawakuisikia ile sauti”.

Jee! ni kweli Paulo ni nabii?

Mtume lazima awe mkweli na mcha Mungu kuanziya utotoni. Swali linakuja Paulo ni mkweli?

Matendo ya Mitume: 22:1-5 Enyi wanaume, ndugu zangu na baba zangu, nisikilizeni, nikijitetea mbele yenu sasa. 2 Waliposikia kwamba anasema nao kwa lugha ya Kiebrania wakazidi kunyamaza; akasema, 3 Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, ila nililelewa katika mji huu, miguuni pa Gamalieli, nikafundishwa sheria ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa jitihadi kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi; 4 nikawaudhi watu wa Njia hii hata kuwaua, nikawafunga, nikiwatia gerezani, wanaume na wanawake.

Acts:22:3. I am verily a man which am a Jew, born in Tarsus, a city in Cilicia, yet brought up in this city at the feet of Gamaliel, and taught according to the perfect manner of the law of the fathers, and was zealous toward God, as ye all are this day

Katika aya hizi kuna uthibitisho wa kuwa yeye Paulo ni Mtu wa Kiyahudii mzaliwa wa Tarso, mji wa Kilikia

Warumi: 11:1-3 Basi, nauliza, Je! Mungu aliwasukumia mbali watu wake? Hasha! Kwa kuwa mimi nami ni Mwisraeli, mmoja wa wazao wa Ibrahimu, mtu wa kabila ya Benyamini.

Mdo ya mitume: 16:38. Wakubwa wa askari wakawapasha makadhi habari za maneno haya; nao wakaogopa, waliposikia ya kwamba hao ni Warumi.

Paulo hakuwa Myahudi, bali ni Mrumi.

    • MDO 22:27 (SUV)

      Jemadari akaja, akamwuliza, Niambie, u Mrumi? Akasema, Ndiyo.

    • MDO 22:27 (SUV)

      Jemadari akaja, akamwuliza, Niambie, u Mrumi? Akasema, Ndiyo.

      • MDO 22:26 (SUV)

        Yule akida aliposikia, akaenda akamwarifu yule jemadari, akisema, Unataka kufanya nini? Kwa maana mtu huyu ni Mrumi.

      • MDO 22:28 (SUV)

        Jemadari akajibu, Mimi nalipata wenyeji huu kwa mali nyingi. Paulo akasema, Na mimi ni Mrumi wa kuzaliwa.

Farisayo

 

  • MDO 23:6 (SUV)

    Paulo alipotambua ya kuwa sehemu moja ni Masadukayo, na sehemu ya pili ni Mafarisayo, akapaza sauti yake katika ile baraza, Ndugu zangu, mimi ni Farisayo mwana wa Farisayo; mimi ninahukumiwa kwa ajili ya tumaini la ufufuo wa wafu.

  • FLP. 3:5 (SUV)

    Nalitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benyamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo,

  • THE WARNING FROM JESUS CHRIST:
    • MT. 5:20 (SUV)

      Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. Kuhusu Hasira

 

Warumi: 7:14 Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni; bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi. 15Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda. 16Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema. 17Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu 18Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati. 19Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo.

Kati ya Paulo na Yesu ni nani Mwenye Uwezo Zaidi?

Yesu amesema:

Mathayo: 15:24. Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. 

 Paulo anasema:

Warumi: 11:13.Lakini nasema na ninyi, mlio watu wa Mataifa. Basi, kwa kadiri nilivyo mtume wa watu wa Mataifa, naitukuza huduma iliyo yangu,

Yesu anasema:

  • MT. 10:8 (SUV)

    Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.

 

Paulo anasema:

 

  • 1 KOR. 9:14 (SUV)

    Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili.

Paulo anasema:

Tito:2:13.tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;

 

Yesu anasema:

  • YN. 14:28 (SUV)

    Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba, kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi.

Paulo Kamtukana Mungu

1Wakoritho:1:25. Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.

Paulo anasema ya kwamba yeye si mkweli.

Warumi: 3:7. Lakini, ikiwa kweli ya Mungu imezidi kudhihirisha utukufu wake kwa sababu ya uongo wangu, mbona mimi ningali nahukumiwa kuwa ni mwenye dhambi? 

Kutahiriwa

Luka:2:21

Hata zilipotumia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu; kama alivyoitwa na malaika kabla hajachukuliwa mimba

Lakini Paulo anapiga sheria ya kutahiriwa

Wagalatia: 5:2 Tazama, mimi Paulo nawaambia ninyi ya kwamba, mkitahiriwa, Kristo hatawafaidia neno.

Leave a comment